| by Rajabu mrisho | No comments

NJIA KUU NNE ZA KUWA TAJIRI

1.KUAJIRIWA
-Njia hii ndio inafahamika na watu wengi. Wengi wanasoma wakitegemea waje waajiriwe.

Faida za njia hii.
-Ndio njia nyepesi ya mtu kujipatia kipato cha halali.

Changamoto zake.
-kwa zama hizi vijana wanao maliza vyuo wamekuwa wengi sana hivyo swala la kuajiliwa limekuwa kama bahati nasibu hiyo yote ni kwa sababu zama zimebadilika tupo zama za taarifa.
-Ni njia ambayo haiwezi kumfanya mtu kuwa tajiri kwa haraka.
-Ni njia ambayo itahitahi muda wako mwingi kuwa kazini.
-Ni njia ambayo mfanyakazi analipa kodi kubwa.

2.KUJIAJIRI.
-Ni njia ambayo inajumuisha wafanya biashara wadogo wasanii nyota wa michezo, filamu n.k
-Jamii kubwa ya Watanzania ambao hawaja ajiriwa ni wajasiliamali wadogo /wamejiajili.

Faida za njia hii.
-Ni njia ambayo unakuwa na usimamizi wote wa biashara yako.

Changamoto zake.
-Ni njia ambayo mfanyakazi analipa kodi kubwa mfn TRA.
-Ni njia ambayo itatumia muda wako mwingi.
-Ni njia ambayo inawafanya watu wengi kuona kuwa biashara na uwekezaji ni hatari.
-kama huna ujuzi ina weza kuwa hatari, kupunguza hatari ijue zaidi biashara yako.

3.BIASHARA KUBWA /MJASILIAMALI
Biashara kubwa ni biashara ambazo zina wafanya kazi wengi.
-Tofauti kati ya biashara kubwa na ndogo ni kwamba wafanya kazi wa biashara ndogo ni watu wa nyumbani lakin biashara kubwa ni watu Tofauti.

Faida za njia hii.
-Njia hii inaweza kukufanya kuwa tajiri kwa haraka zaidi kwa sababu inahusisha watu wengi.
-inakupa uhuru wa kufanya mambo mengine kwa sababu unawatu wanafanya kazi kwa ajili yako
-kupitia njia hii unalipa kodi kidogo.

Changamoto zake.
-ujuzi unahitajika

4.KUWEKEZA
-Hii ni njia ambapo mtu anawekeza katika mradi fulani kwenye biashara kubwa na ndogo ndogo.
-kupitia njia mtu anakuwa na pesa zinazo fanya kazi kwa ajili yake.

Faida za njia hii.
-inaampa mtu uhuru kwa sababu anapesa zinazo fanya kazi kwa ajili yake
-mtu hulipa kodi kidogo au halipi kihalali.
-humfanya mtu kuwa tajiri kwa haraka zaidi.

Changamoto zake.
-inahitaji ujuzi
-inahitaji mtaji.

Kupitia group hili tutaelezea zaidi jinsi ya kuwa mjasiliamali. Usisahau ku share ujumbe huu

Leave a Reply

avatar
  Subscribe  
Notify of