| by Rajabu mrisho | No comments

MTAZAMO POTOFU JUU YA UTAJIRI

MTAZAMO POTOFU JUU YA UTAJIRI
Je, unahitaji kuwa tajiri? Tajiri wa mali, akili na kuongeza upendo kwenye mahusiao na kufanikwa kwenye maisha?

Ili uweze kuwatajiri na kufanikwa kwenye maisha, kwanza inatakiwa uelewe baadhi ya mitazamo ya jamii juu ya utajiri na mafanikio kisha ubadili mtazamo wako. Zifuatazo ni baadhi ya mitazamo ya jamii juu ya utajiri na mafanikio.

1.UTAJIRI NA UCHAWI./USHIRIKINA
-Watu wengi wana dhana ya kwamba ili uwe tajiri lazima uwe mchawi au mshirikina kama vile kutoa kafara ndugu wa karibu.
-Jamii kubwa ya watanzania ina amini yafuatayo :
a. pesa za majini : Ili uwe tajiri lazima uwe na majini ambayo yatakuwa yanakupa pesa muda utakao kuwa unahitaji, wengine wanaamini mpaka uwe na chuma ulete.
Misukule kwenye biashara : wengine wanaamini ili uwe tajiri lazima uwe na Misukule ambayo itakuwa inakuletea wateja kwenye biashara yako.
Uchawi kwenye ndoa : wengine wanaamini ya kwamba ili mwenza wako aweze kukupenda lazima umroge au umpe limbwata.
Pete za majini: wengine wanaamini ya kwamba ili uweze kuwa tajiri lazima uwe na Pete ambayo itakupa kila kitu pale utakapo iomba.
Tarasimu : huu ni Uchawi wa maandishi/kiarabu ambao waty huutumia kupata utajiri na mafanikio.
Je, niupi mtazamo sahihi juu ya utajiri na Uchawi /ushirikian?
Uchawi/ushirikiana haumfanyi mtu kuwa tajiri, wala hauongezi furaha kwenye familia wala haupelekei mafanikio, isipo kuwa humfanya mtu kuwa mtumwa wa majini badala ya kumtegemea muumba wake.
Ili uweze kuwatajiri na kufanikwa, kwanza inatakiwa ubadili Mtazamo wako juu ya uchawi na ushirikiana. Inatakiwa uaimini kuwa unaweza fanikiwa bila kutumia uchawi au ushirikiana.

2.UTAJIRI NA UTJIRI/UKABILA/RANGI
-Watanzania wengi wanadhana ya kwamba ili uweze kufanikwa katika maisha au mahusiano lazima uwe unatoka nchi fulani, kabila fulani au uwe na rangi fulani.
-Jamii kubwa ya Watanzania ina mitazamo ifuatayo,
Ili uweze kuwatajiri lazima uwe na rangi nyeupe au ulizaliwa nchi zy magharibi, wengine mpaka wakafikia kusema “bora ninge zaliwa mbwa ulaya ila sio bongo”
Wengine wanaamini ili wapate mahusiano au ndoa yenye furaha lazima waoe au waolewe na watu wa kabila au rangi fulani.
Wengine wanaamini biashara kubwa haziwezi fanikiwa afrika.
Wengine wanaamini kwa sababu wamezaliwa afrika, hawawezi kuwa matajiri.

Je, ni upi mtazamo sahihi juu ya utajiri na utaifa au rangi au ukabila?
Kwanza inatakiwa uelewe kwamba kuzaliwa maskiini afrika au kuzaliwa kwenye kabila fulani sio Kosa, ila Kosa ni jinsi wewe unavyo jidharau na kujishusha hadhi yako.
Wapo waafrika wengi waliofanya mambo makubwa duniani, unashindwaje na wewe kuwa mmoja wao? Mfano Mansa Musa ambaye ndio tajiri mkubwa historia, pia Elon Musk wa South afrika.
Hivyo ili uweze kufanikwa usijidharau kwa nchi uliyo zaliwa, kwa rangi uliyo nayo, inatakiwa uaimini kuwa unaweza.

Leave a Reply

avatar
  Subscribe  
Notify of